Listen to this post:
"Sikiliza ndugu yangu, hapa DSN hatupendi kukupiga maneno mengi. Leo ngoja nikwambie kitu kimoja muhimu sana — kitu kinachoitwa HTML. Kama unataka kuingia kwenye ulimwengu wa kutengeneza websites, lazima ukifahamu hiki kitu. Sasa, hebu tusonge pamoja hatua kwa hatua."
✅ HTML ni nini?
HTML ni kifupi cha HyperText Markup Language. Hii ni lugha ambayo inatumika kuandika na kupanga muundo wa kurasa za tovuti (webpages).
Kwa mfano, unapotembelea website yoyote — iwe ya DSN, YouTube, Google au hata blogu ya rafiki yako — browser inatumia HTML kuonesha maandishi, picha, video, links na kila kitu unachokiona.
๐ HTML hufanya kazi gani?
HTML inasema:
- Hapa ni kichwa cha habari
- Hii ni paragraph ya maelezo
- Hapa weka picha
- Hii ni link ya kubonyeza
- Hapa weka jedwali, fomu au button
Yaani ni kama inatoa maelekezo kwa browser jinsi ya kupangilia kila sehemu ya ukurasa wa mtandao.
๐ง Hebu tujifunze mfano moja hapa hapa:
<!DOCTYPE html>
<html>
<head>
<title>Karibu DSN</title>
</head>
<body>
<h1>Habari na Karibu DSN Technology</h1>
<p>Sisi ni wataalamu wa teknolojia, tunafundisha na kutengeneza websites.</p>
<a href="https://dsn.co.tz">Tembelea tovuti yetu</a>
</body>
</html>
Maelezo ya Kifupi:
<!DOCTYPE html>
➜ Inaiambia browser kwamba huu ni ukurasa wa HTML5.<html>
➜ Hii ni mzizi wa ukurasa wote.<head>
➜ Hii sehemu huweka vitu vya ndani kwa ndani kama jina la ukurasa.<title>
➜ Jina linaloonekana juu kabisa kwenye tab ya browser.<body>
➜ Ndani yake kuna mambo yote yanayoonekana kwa mtumiaji.<h1>
➜ Heading kubwa, kwa mfano kichwa cha habari.<p>
➜ Paragraph — maelezo au sentensi za kawaida.<a href="...">
➜ Link ya kubonyeza inayopeleka sehemu nyingine.
๐ค Kwa nini ujifunze HTML?
"Ndugu yangu, kama unataka kuwa mtu wa tech, unayetengeneza websites zako mwenyewe, unayetengeneza huduma za mtandaoni kama DSN Online, basi HTML ni hatua ya kwanza."
Na nzuri zaidi ni kwamba:
- HTML ni rahisi kujifunza
- Unaweza kufanya bila kuwa na kompyuta kubwa
- Inakupa msingi wa kufahamu CSS, JavaScript, na frameworks kama React
๐ฃ Karibu DSN Technology
Hapa DSN tunakufundisha HTML kwa lugha rahisi kabisa — kwa vitendo, kwa simu au kompyuta, bila stress. Tunataka uwe mtaalamu, siyo mtazamaji tu.
๐ง DSN — Minds Behind the Machines
๐ฒ Wasiliana nasi kwa kozi za tech, websites, na huduma za kiteknolojia.