Karibu kwenye dunia ya hela za mtandaoni! Wakati watu wengine wanapiga picha za chai na chapati za asubuhi Facebook, wewe utajua siri ya kulipwa kwa kutumia platform hiyo hiyo. Sasa hebu tuingie kwenye nyama ya somo, lakini usijali – hakuna kuotea wala kutumiwa link za kutapeliwa. Hapa ni mbichi mbichi!
1. Kwanza kabisa – Facebook inalipa vipi?
Kabla hujaanza kufikiria kuhusu kununua gari ya ndoto zako kupitia Facebook, ni vizuri kujua kwamba Facebook inalipa watu kupitia mfumo unaoitwa Meta Monetization. Ndiyo, Meta ni jina jipya la kampuni mama ya Facebook. Sasa wana mfumo maalumu wa kulipa content creators kwa njia kuu kama hizi:
In-Stream Ads (Matangazo ndani ya video zako)
Stars (Mashabiki kukutumia zawadi wakati wa live)
Reels Play Bonus Program
Affiliate Marketing (Kwa wale janja wa kuuza bidhaa)
Brand Partnerships (Makubaliano na kampuni mbalimbali)
Lakini kabla hujaruka mduara wa furaha, kuna masharti.
____________________
2. Masharti ya kuwa eligible (usikate tamaa hapa)
Facebook siyo mama yako, haina huruma ya kukulipia bure. Hizi hapa ndizo nguzo za chuma unazopaswa kuzikamilisha:
Uwe na page (siyo akaunti ya kawaida tu!)
Page yako iwe na angalau followers 5,000
Angalau dakika 60,000 za watu kutazama video zako ndani ya siku 60
Video zako lazima ziwe Original – hakuna kuiba YouTube ya watu halafu unaweka Facebook
Hapo sasa, kama uko mbali bado, usihofu – kuna njia za mkato halali. Nitakueleza.
_______________________
3. Njia za mkato za halali (siyo shortcut za kichawi, hizi ni mbinu legit)
a) Fanya mahojiano na watu mashuhuri wa mtaani
Hii njia iko underrated! Kamata fundi wa boda maarufu mtaani, msusi wa “full figure” au mama ntilie anayejua kupiga story. Waulize maswali ya maisha halafu upost video hizo kwenye page yako. Watu wanapenda realism kuliko content ya Hollywood.
b) Tengeneza Reels zenye utani wa kitaani
Mtu akiona video yako anatabasamu? Uko njiani kuwa millionaire wa Facebook. Reels ndizo zinapata attention sana. Zitengeneze, zishare, na usiogope kuonekana ‘simple’ – watu wanapenda kuwaona watu wa kawaida wakifanya mambo ya kawaida kwa njia isiyo ya kawaida.
c) Live sessions na mashabiki wako
Hapa ndipo unapoweza kuanza kupata Stars – watu wakikupenda, watakutumia hizo stars ambazo Facebook huzilipa kwa dola. Huna haja ya kusubiri mshahara wa mwezi mzima kutoka serikalini – hapa ni papo kwa papo.
_________
4. Baada ya kupata viewers na masharti – sasa inakuaje?
Meta Creator Studio ndio ofisi yako. Ukiingia hapo, utaona kama ume qualify kwenye monetization. Kama bado, itakuambia unahitaji nini. Ukiqualify, basi utachagua jinsi ya kulipwa:
PayPal
Bank Transfer (direct kwa akaunti yako ya benki)
Payout thresholds – lazima ufikishe kiwango fulani (mfano $100)
_________________
5. Siri ya mafanikio – consistency + creativity
Kama ulidhani utaweka video mbili kisha ukafunguliwa line ya M-Pesa na Mark Zuckerberg mwenyewe, pole. Ni lazima uwe consistent – yaani unapost content mara kwa mara. Pia uwe mbunifu – watu wakiona content zako ni za kuchosha, watapita tu kama vile hawajakuona.
Ushauri wa bure: Usijifananishe na watu wakubwa kama The Wabebe Show au Nas Daily siku ya kwanza. Anza taratibu, ukikosea video mbili usijifutie page – hata Yesu hakuanza kuwa maarufu siku ya kwanza!
_______________________
6. Bonus: Vitu 3 visivyosemwa na wengi kuhusu kulipwa na Facebook
1. Unaweza kulipwa hata kama uko Afrika Mashariki – Mradi umeweka njia sahihi za kulipwa.
2. Facebook huwa na bonuses za ghafla – unaweza ukapewa dola 500 tu kwa kuwa na reels kali sana.
3. Mashabiki wanaweza kukununulia Stars hata kama wewe hujui – ndiyo maana unahitaji kuwa live mara
Ukiamua, unaweza!
Facebook siyo tena app ya kutazama picha za harusi za watu – ni duka la hela, jukwaa la mafanikio, na benki ya ubunifu. Lakini kama kawaida, hakuna mafanikio bila juhudi. Ukiamua leo, ukaanza kuweka content bora, ukaweka consistency, ukaelewa jinsi ya kutumia Creator Studio, basi Facebook itakulipa.
Kumbuka: Wale wanaocheka post zako leo, wataomba shoutout kesho!
______________________________
Unapenda post kama hizi? Fuatilia DSN TECHNOLOGY kila wiki kwa mbinu halisi, ushauri wa kweli na siri ambazo hazipatikani Google wala YouTube!